YA DITO, NDUGU ZAKE, DHAMANA NA MAHAKIMU!!!
Juma hili linamalizika huku mawaziri wanaohusika na usalama na haki za raia wakishindwa kuwashawishi mahabusu amabo wamekuwa wakigoma sasa mpaka nao kesi zinazowakabili mahakama zitasikilizwa kwa haraka kama ilivyotokea kwa mtuhumiwa wa kesi ya kukusudia kuua ndugu Ditto amabye kesi yake imechukua miezi mitatu tu na sasa yupo nje kwa dhamana kwani kosa lake lina dhaminika ilhali mahabusu wengi wakiwa gerezani kwa takribani miaka10 mpaka 15 kesi zao zikitajwa tu bila chochote kuendelea.
Wamegoma!
Nawashangaa sana hawa mahabusu amabo wameamua kugoma ili kushinikiza kesi zao ziharakishwe kama inavyotokea kwa kesi zinazowakabili vigogo ama watoto wao ama watu maarufu. Kesi zinatofautiana na watuhumiwa wanatofautiana sana kwani hata binadamu wote si sawa japo katiba yetu inayoongozwa na mfumo wa ujamaa kutamka kuwa binadamu wote ni sawa.
Kesi inayoendelea ya mheshimiwa inadhihirisha yale G. Orwell aliyosema katika kitabu chake maarufu kinachoitwa 'the animal farm' shamba la wanyama kuwa kuna binadamu wengine ni zaidi ya wengine.
ninakuwa ninajiuliza kuwa inawezekana ni mfumo wetu wa sheria una macho ama watendaji wenye dhamana ndio wanaoangalia na kuifanya sheria kuwa na macho na kuipotezea imani yake kuwa sheria ni msumeno!
Nimemshangaa jaji mkuu amabye ameshangazwa na kitendo cha wasalama kumpitisha kigogo katika mlango unaotumiwa na mahakimu, hivi hajui kuwa watuhumiwa wengine ni mahakimu tayari, kwenda mahakamani kwao ni kama kuwazuga tu na ndiyo maana wakati wanaogoma wanarundikwa kwenye makarandinga wao wanaletwa na taksi amabyo inalindwa na polisi wenye silaha ili kutotota nafasi kwa 'washenzi' kutotoa habari kwa umma.
Najiuliza wale ndugu wa mtuhumiwa waliowafanyia uhuni wapigapicha wa habari corparation walikuwa wanajua kuwa ni lazima ndugu yao atapewa dhamana! Hivi kama hakimu angekataza dhamana nani angeshambuliwa na ndugu hawa amabo mahakama waliifanya kama sehemu ambako mwali anatolewa kwa kwenda na kanga huku walinzi wa usalama wakiwaangalia kana kwamba wanachofanya kinaruhusiwa.
Ingekuwa ni 'kapuku' kweli angeruhusiwa kwenda hata na 'leso' ikiwa tu simu ya kapuku ikiita basi hima askari atakufuata na kukugombeza huku hakimu akitishia kukuadhibu kwa kuleta kelele kortini.
Sheria haina macho lakini waliodhaminiwa na wanachi kuitunza na kuiimarisha wamekuwa wabaguzi huku vigogo wakikrimiwa na walalahoi wakinyanyaswa hata kwa kufanya mepesi dhidi ya mazito yanayofanywa na vigogo
2 comments:
Obe!
Ukiwa maskini katika Tz ya leo sahau kupata haki yako hata kama sheria iko upande wako>Tazama vigogo wanavyotuhumiwa na makosa makubwa na bado wanaachiwa huru tena na vyombo tunavyoviaminia kwa kutoa haki
Kesi hizi zinashangaza sana, nina ndugu yangu ambaye alituhumiwa kufadhili mauaji, leo ni mwaka wa nne yupo rumande huko mkoani. Nina imani angekuwa ni kigogog basi hata kesi isingekuwapo kwani tunaelewa jinsi wanavyoshiriki kupanga mauaji ya watu mbalimbali na wala hakuna anayewaleta mahakamani hata kama dola inafahamu
Post a Comment