Monday, December 27, 2010

Saturday, October 23, 2010

Tujiandae na Uchaguzi MKUU

Kura yako ndiyo kila kitu katika kuleta maendeleo, hivyo piga KURA kwa busara na acha woga kwani AMANI BILA HAKI ni kama jua bila mawingu

Wednesday, September 01, 2010



JOHN MNYIKA AZINDUA KAMPENI ZA UBUNGE CHADEMA UBUNGO

Dr Wilbroad Slaa mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA akimnadi John Mnyika kwa wananchi wa Jimbo la Ubungo ,alipokuwa akihutubia katika ufunguzi wa Kampeni za CHADEMA Ubungo juzi Jumapili Kimara Suca.

Vijana wa kazi Mkoloni na Mr II (SUGU) wakilishambulia jukwaa la ufunguzi wa kampeni za Mnyika Kimara Suca(kwa hisani ya blog la fullshwange)

TENDWA KUTOA MAAMUZI PINGAMIZI LA CHADEMA BAADA YA SIKU TANO!

 
 
Na Mary Kweka –Maelezo
Msajili wa Vyama Vya Siasa Nchini John Tendwa amesema atatoa uamuzi wake dhidi ya malalamiko yaliyowasilishwa ofisini kwake jana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA)kuhusu mgombea wa urais kupitia chama cha mapinduzi(CCM) baada ya siku tano.
Bwana Tendwa ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari hayo ofisini kwake jijini Dar es salaam baada ya kupokea malalamiko hayo rasmi leo.
‘’Nitatoa maamuzi hayo baada ya kupokea maelezo kutoka kwa mlalamikiwa dhidi ya malalamikaji yaliyowasilishwa,na nitatoa nakala ya maamuzi kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi,Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi na Katibu Mkuu wa chama cha CHADEMA’’,Alisema Tendwa.
Akifafanua suala hilo Tendwa amesema baada ya maamuzi yake mlalamikaji na mlalamikiwa kama hawataridhika na uamuzi wake wanayo haki ya kwenda kutafuta haki yao kwenye vyombo vya sheria.
Aidha Msajili huyo Vyama ameongeza kuwa amepokea malalamiko hayo kwa mujibu wa sheria ya gharama za uchaguzi inachomkataza mgombea yeyote ambaye yeye mwenyewe, wakala wake au Chama chake kitafanya kitendo ambacho kimekatazwa kama ilivyoelekezwa kwenye sheria hiyo atakuwa au kitakuwa kimepoteza sifa za kushiriki mchakato wa uteuzi au uchaguzi.
Pingamizi hilo liliwasilishwa jana ofisi ya masajili huyo na Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika wakimlalamikia Mgombea urais wa chama cha mapinduzi Jakaya Mrisho Kikwete kutumia madaraka yake kutoa ahadi kwenye kampeni na kutangaza nyongeza ya mshahara kwa wafanyakazi wakati wa kampeni.

Sunday, August 29, 2010

Picha Za Uzinduzi wa Kampeni ya Chadema

Chadema Wazindua Kampeni Zao Jangwani Leo

Nimebahatika kuhudhuria mkutano wa uzinduzi wa kampeni wa Chadema na kupta baadhi ya picha ambazo nimezipandisha hapa na nyingine ni kwa hisani ya wanablog kina Michuzi na Jamii orums



Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dr. Willbrod Slaa akizungumza jana jioni wakati wa uzinduzi wa kampeni na ilani ya chama chao mbele ya maelfu ya watu waliofika kuushuhudia uzinduzi huo katika viwanja vya jangwani. Dr Slaa alisema kuwa akipewa ridhaa ya kuiongoza nchi hii basi atahakikisha ndani ya siku 100 za kwanza,katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania inafanyiwa marekebisho makubwa na pia kuhakikisha mfumo wa Elimu hapa nchini unabadilishwa kabisa.

"MTOTO ACHWEKWAYE NDIYE AKUAYE" ni msemo aliotoa Mgombea Mwenza wa Dr. Willbrod Slaa,Said Mzee wakati akiwahutubia wanachama na wapenzi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliofika katika viwanja vya Jangwani jana. .

Mgombea Urais wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dr. Willbrod Slaa akimtambulisha rasmi mke wake aitwaye JJosephine mbele ya maelfu ya watu waliofika kwenye uzinduzi wa kampeni na ilani ya chama hicho jioni ya jana katika viwanja vya jangwani,jijini Dar.

Mwenyeki wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman Mbowe akikabidhi vitabu vya Ilani ya chama hicho kwa mgombea Urais wa chama hicho Mh Willbrod Slaa jana  jioni katika viwanja vya Jangwani jijini Dar mara baada ya kuizindua.

Mwenyeki wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman Mbowe akionesha vitabu vya Ilani ya chama chao mara baada kuizindua katika viwanja vya Jangwani,jijini Dar.

Muasisi wa vyama vingi nchini na Mwenyekiti wa kwanza wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Mabere Marando ambaye pia amejiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),akionesha kitabu cha Ilani ya chama hicho mbele ya Wananchi waliofika katika viwanja vya jangwani leo.Marando aliongeza kwa kusema kuwa siku ya Jumatatu wataweka pingamizi kwa mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mh Dr. Jakaya Kikwete kwa kudaiwa kukiuka baadhi ya sheria za Uchaguzi.

Aliyekuwa Mgombea Ubunge kwa tiketi ya chama cha CCM,na baadae akahamia chama cha CHADEMA hivi karibuni,John Shibuda akizungumza mbele ya wananchi  wakati chama hicho kilipokuwa kikizindua kampeni na Ilani yake katika viwanja vya Jangwani na kuhudhuriwa na mamia ya watu.

Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya na Mgombea Ubunge kwa tiketi ya chama cha CHADEMA jimbo la Mbeya mjini,Joseph Mbilinyi a.k.a Mr II a.k.a Sugu akiimba moja ya nyimbo zake ujulikanao kwa jina la ‘Sugu’ ambao ulionekana kuwachangamsha vijana wengi waliofika viwanjani hapo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya chama hicho pamoja na Ilani yake.

Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na mgombea Ubunge wa jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lisu akiwahutubia wanachama wa Chadema waliofika katika viwanja vya jangwani  huku akiwa ameshika kitabu alichokisema kuwa ni moja ya mikataba ya migodi.

Mwenyeki wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman Mbowe akijaribu kuwatuliza baadhi Wananchi kuwa wawe na utulivu hakuna kitakachoharibika,Mbowe ilibidi awatulize Wananchi mara baada kubaini kuwa shirika la utangazaji la TBC1 lilikatisha matangazo ya uzinduzi wa kampeni ya chama hicho yaliyokuwa yakirushwa LIVE na hata kuthubutu kutaka kumpiga mmoja wa watangazaji wa kituo hicho, na baadae TBC1 waliamriwa waondoke uwanjani hapo kwa usalama wao.

Mgombea Urais kwa Chama cha CHADEMA,Mh.Willibrod Slaa akiwapungia wananchi mbalimbali waliofika kwenye viwanja vya Jangwani mara ya kushuka kwenye gari.

"AIBU" shirika la umma ambalo kikundi cha watu wachache wanadhani ni mali yao binafsi. Mtangazaji wa Mahiri wa TBC1 Marin Hassan Marin akisindikizwa na askari ili kujaribu kuzuia lolote baya lisimkute wakati wakielekea kwenye gari kwa lengo la kuondoka kabisa eneo la tukio,hata hivyo baadhi ya wananchi waliokuwa na jazba ya tukio hilo waliendelea kulalama mpaka Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA,Freeman Mbowe aliposimama na kuwasihii wananchi watulie na amani itawale eneo hilo la jangwani,na kweli baadae hali ikawa shwari na uzinduzi wa kampeni ukaendelea.

maelfu ya wanachadema waliofika katika viwanja vya jangwani .

Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jimbo la Kawe,Halima Mdee akipitisha bakuri la kuomba msaada kutoka kwa watu mbalimbali waliofika viwanjani hapo,fedha hizo ambazo imeelezwa kuwa zitatumika kwenye mbio za kampeni ambazo wamezindua  na wanatarajia kuzianza hivi karibuni Tanzania nzima.

Msanii G- Solo akishambulia jukwaa .

Msanii wa Bongofleva Dani Msimamo akiimba jukwaani.

Mmoja wa Wasanii wa muziki wa kizazi kipya,Mkoloni ambaye pia ni Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akisoma risala fupi kwa niaba ya Wasanii wenzake kuhusiana na mambo mbali mbali yanayoikumba anga ya muziki na wanamuziki wenyewe,Mkoloni baadae lisala hiyo aliikabidhi kwa mgombea Urais wa chama hicho Dr.Willbroa Slaa.

WanaChadema wakiwa juu ya mti ili kuweza kuona na kusikia kila kinachoendelea katika viwanja vya jangwani.

Askari Polisi wakituliza ghasia zilizotaka kuletwa na wanachama wa Chadema katika gari la kurushia matangazo la Television ya Taifa TBC.

Gari la matangazo la TBC baada ya kuwekewa uilnzi ili lisiletewe fujo na wanachama wa Chadema.

Mkutano ukiendelea.

walielekea jukwaa kuu.

gari lililommbeba mgombea urais wa Chadema likiwasili katika viwanja vya jangwani .

moja ya vioja vilivyokuwepo katika viwanja vya jangwani

umati wa wanachademana wananchi waliohudhuria mkutano wa uzinduzi wa kampeni

Friday, August 27, 2010

MAMISS WA SIKU HIZI KWA MIWANI..!!

                                                                           

                                            
  Baadhi ya washiriki wa Vodacom Miss Tanzania wakiwa na miwani kitu ambacho kimekua kivutio kikubwa kwa mamiss,kiukweli zinawapendeza na kuwaongezea nakshi  mida frlani hivi....
                                                     
                                                                           

TIGER WOODS NA MKEWE WATALIKIANA.

BINGWA WA MCHEZO WA GOLF DUNIANI TIGER WOODS AMETALIKIANA NA MKEWE ELIN NORDEGREN. HIZI NI HABARI KUTOKA MTANDAO WA MCHEZAJI GOLF NAMBA MOJA DUNIANI.

KWA PAMOJA WALISEMA "Tunasikitika kuwa ndoa yetu imefikia tamati na tunatakiana kila la heri katika mustakabala wetu," WAWILI HAO WALISEMA.


HATA HIVYO WAWILI HAO WAMESEMA WATASAIDIANA MAJUKUMU YA KULEA WATOTO WAO WAWILI. SUALA LA KUGAWANA PESA HALIJAWEKWA WAZI LAKINI TAARIFA KATIKA VYOMBO VYA HABARI VYA MAREKANI ZINASEMA KUWA BI.NORDEGREN HUENDA AKAONDOKA NA KITITA CHA DOLA MILIONI 100.

                                                 
                                      Bata za jigga na beyonce ni za hal ya juu mmmh..
                                          
kundi la Wanaume (lililojiengua kutoka kwa kundi la Wanaume Halisi) linatarajia kuitambulisha albamu yake mpya itakayokwenda sambamba na uzinduzi wa Logo pamoja na tovuti yao kwa watu maalumu ndani ya kiota cha maraha kilichopo kati kati ya jiji,Savanah Lodge mnamo Octoba 25.

Akizungumza na Jiachie jijini Dar jioni hii kiongozi wa kundi hilo Rich One amesema kuwa baada kuikamilisha albamu yao yenye jumla ya nyimbo kumi,kwa sasa wanajipanga vyema kuitambulisha albamu hiyo itakayojulikana kwa jana la POA TUA, vile vile utakwenda sambamba na uzinduzi wa Logo na tovuti itakayokuwa na habari zao mbalimbali zikiwemo na kazi zao kama vile vyimbo na video zao.

"Tumeamua kuja na mambo mapya baada ya kimya kidoogo kwa wapenzi wetu,kama nilivyosema hapo awali albamu ina jumla ya nyimbo kumi,ambazo baadhi yake ni Poa Tu, Mapenzi Matamu, Apple, Moyo Wangu, Zaga Zaga na nyingine nyingi," alisema Rich One na kuongeza kuwa albamu hiyo imesheheni mahadhi tofauti tofauti kama vile Zouk, R&B pamoja na Hip Hop.

Rich One amesema kuwa ndani ya albamu hiyo amewashirikisha wasanii kadhaa mahiri katika anga ya muziki wa kizazi kipa,kama vile Chidi Benz,Kitokororo wa FM Academia,Hard Mad,Chiku Keto,Mh Themba na wengineo.

Kundi hilo linaloundwa na wakali akiwemo Athuman Yahya (A.Man), Juma Mbelwa (Juma Jazz), Karim Kaiman (Kakaman), Abdul Ally (Mzimu), Richard Shauri (Rich One) pamoja na David Mpangile (Da
Mama Salma Kikwete
NA MWANDISHI MAALUM, RUFIJI

WANAWAKE wanaokopa kutoka taasisi za fedha, wamekumbushwa kuzingatia masharti ya mikopo ikiwa ni pamoja na kuirejesha kwa wakati kuwezesha wengine kutumia fursa hiyo.
Akizungumza na kina mama wa wilaya za Mkuranga, Bagamoyo na Rufiji, mkoani Pwani, Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete, alisema kukopa fedha na kutozirejesha ni kukwamisha jitihada za wengine ambao nao wanazitaka kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi.Mama Salma alisema kwamba, mtu anapokopa fedha kwa ajili ya kutekeleza mradi, ahakikishe anazitumia kwa kazi hiyo na sio vinginevyo.

"Kina mama wenzangu, mkopo ni mkopo, lengo lilokufanya uchukue mkopo ni mradi wa kujiletea maendeleo, usitumie fedha za mkopo kununua doti za khanga, huko ni kujisababishia matatizo bila sababu za msingi," alisema.

Alifafanua kwamba, serikali ya awamu ya nne ilipoingia madarakani ilikuwa na kauli mbiu ya maisha bora kwa kila Mtanzania, na fursa ya kupata mikopo, inalenga katika kuwezesha kauli mbiu hiyo kutekelezeka.

Mama Salma aliwasisitizia wanawake kuendelea kujiunga na vyama vya kuweka na kukopa (SACCOS) na VICOBA, ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kupata fedha za mikopo kwa ajili ya kuendeleza na kuanzisha miradi ya uzalishaji mali.

Kuhusu elimu, alisema mataifa yote yaliyoendelea, yamewekeza katika elimu ya watoto wao ndiyo maana serikali chini ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete katika miaka mitano yakuwepo madarakani, iliamua kujenga shule nyingi za sekondari na kupanua elimu ya vyuo na vyuo vikuu.
Huku akiwaomba kina mama hao kumpigia kura mgombea urais wa CCM Rais Jakaya Kikwete na wagombea wa ubunge na udiwani wa chama hicho katika uchaguzi mkuu ulipangwa kufanyika Oktoba 31, mwaka huu, Mama Salma alisema miaka ya sasa siyo ya kupuuzia elimu.

"Nchi yoyote yenye mafanikio imewekeza vyema katika elimu ya watoto wao, nasi hatuwezi kubaki nyuma katika hilo, shule nyingi tumejenga kwa nguvu zetu na msaada wa serikali, lakini pia tunakabiliwa na changamoto nyingi kuziwezesha kuwa bora zaidi," alisema."Mkikichagua tena Chama Cha Mapinduzi kitafanya kazi hiyo kwa ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi," alisema.
 
hebu angalia hapa kitu wanachokifanya,yaani washasahau kwamba barabara hiyo inatumiwa pia na watu wengine.na hapa ni lazima watakuwa walikuwa wanapiga soga tuu.
uandishi: Othman Michuzi | Tarehe: Wednesday, August 25, 2010
hii ndinga nimekutana nayo mchana wa leo katikati ya jiji la Dar ikiwa imeleta noma (kuharibika) huku jamaa wanaofanya kazi katika gari hilo za usafi wa mazingira wakiwa wamekaa juu ya taka hizo zilizomo ndani ya gari hilo huku wakipiga stori za hapa na pale kana kwamba wapo majumbani mwao vile,tena bila hata wasiwasi.
  


Baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakiangalia Simba anayepita karibu na magari yao wakati warembo hao walipotembelea Hifadhi ya Ngorongoro kujionea wanyama na mambo mbali mbali yalipo katika hifadhi hiyo.
Baadhi ya warembo wanoshiriki mashindano ya Kumsaka Vodacom Miss Tanzania wakicheza ngoma ya Kimasai wakati walipokaribishwa katika Boma la wafugaji hao lililopo ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro wakati wakiwa katika ziara yao ya kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo Mikoa ya Kaskazini, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani.
Baadhi ya Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wakitoka katika nyumba za Tembe za wafugaji wa jamii ya Kimasai waishio katika Hifadhi ya Ngorongoro wakati wakiwa katika ziara yao ya kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo Mikoa ya Kaskazini, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani.
Baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakinunua shanga za kimasai kutoka kwa wauzaji waliopo katika Boma lililopo katika Hifadhi ya Ngorongoro wakati warembo hao walipotembelea hifadhi hiyo wakiwa katika ziara yao ya kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo Mikoa ya Kaskazini, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani.