Wednesday, December 30, 2009

HERI YA KRIMASI WASOMAJI WA MACHWEO

Inawezekana salam hizi zikaja zikiwa ziechelewa, pamoja na hayo bado ni nia yangu kuwatakia heri ya Krismasi kwa mwaka huu wa 2009
SAFU ZA MILIMA YA KITONGA: UZOEFU NA PICHA

Kwa muda wa kama wiki mbili nilikuwa mkoani Iringa kwa ajili ya kushiriki katika michezo inayohusisha taasisi za elimu ya juu na vyuo nchini.

Nilishiriki katika mchezo wa mpira wa wavu, nitajaribu kupandisha picha za michezo hiyo lakini pia nitaweka picha za safu za milima ya Kitonga

Tuesday, June 23, 2009


Jaribu kuangalia upande wa mbele wa Admn blog block, inapendeza

Wednesday, June 17, 2009

JENGO HILI NDIMO TUNATEGEMEA WABUNGE WATUWAKILISHE KIKAMILIFU


BAJETI YA 2009/10



Wakati serikali na Kikwete wakijisifu kwa kuweka kipaumbele katika kilimo, ukweli ni kwamba hakuna jipya linalofanywa na seriakli katika kuhakikisha kuwa kilimo kinakuwa cha kwanza, ni kutumia maneno mazuri kama mawingu makubwa yasiyoleta mvua, huwezi kusema KILIMO KWANZA ilhali umetenga asilimia 6.9 kwa ajili ya kilimo huku AU ikisisitiza angalau kilimo kitengewe asilimia kuanzia 10


Thursday, June 04, 2009


Matangazo kama haya yanalipiwa kodi kweli!

Nadhani Halmashauri zetu na hasa jijini DSM zingeweza kutengeneza pesa nyingi sana kutokana na matangazo haya na yale ya kuongeza Hips na kukrabati matiti ama kumfanya mtu unayempenda naye akupende

MV Magogoni kazini








KIKWETE AZINDUA KIVUKO KIPYA CHA MV. MAGOGONI



Mapema leo mchana rais Kikwete amezindua kivuko kikubwa cha Mv MAgogoni kilichoundwa kwa gharama ya zaidi ya tshs bilioni 8, pesa za wananchi.

Saturday, May 23, 2009

Miaka fulani hivi mkuu alikutana na hawa wasanii

Hapa Mkuu ni kama anasema Cheers Bush


RAIS WA KWANZA TOKA AFRIKA KUKUTANA NA OBAMA


Monday, May 11, 2009

Kikosi cha Taifa Starz kilichopambana na Congo


Kwa mujibu wa TFF, shirikisho la soka nchini lilimwomba Maximo atafute makocha, na hawa ndo aliowaleta. Swali hivi maximo ni kocha ama wakala wa kutafuta makocha

MAXIMO HATUFAI

Wengi unapomwongelea huyu jamaa husingizia kuwa watz wanamwonea wivu, sio kweli maximo hafai kuwa kocha wa timu ya taifa ya Tanzania. Najua msomaji unaweza kutoa mengi, hapa ni changamoto tu na ni wakati wako wewe kuchangia


DIDIER DROGBA
Huyu ni mshambuliaji wa klabu ya Chelsea ambaye henda UEFA ikampa adhabu kwa kumzonga refa wakati wa pambano kati ya Chelsea na Barca. Anatoka Ivory Coast.

Blog hii sasa itakuwa ikipost picha za matukio mbalimbali

Tuesday, January 27, 2009

HIVI MWISHO WA MZAZI MASKINI WA TZ NI NINI!!


Kichwa hapo juu kisikustue na kukutisha, umaskini ninaoungelea hapa sio ule unaojua wewe wa kukosa kula, malazi, hapa naongelea kuhusu uwezo wa umma kufanya maamuzi yao yanaowahusu.

Umma ni tofauti sana na wapiga kura, hawa wapo kwa ajili ya kutunisha matumbo yao. Umma ni zaidi ya watu kwani unahusisha mazingira yao na si kukumbukana kwa baada ya miaka mitano.

Fikiria sakata la vyuo vikuu linaloendelea hivi sasa huku asilimia kubwa ya wanafunzi (wengi wao ni watoto wa wakulima vijijini) ikiwa imekosa udahiliwa mpya uliokuja kama wokovu kwa watoto wa matajiri.

Nadhani ni wakati wa umma kuamka na kutambua kuwa amani bila haki ni kama mawingu bila mvua na siku zote haki hutafutwa. Mustakabali wa Tanzania upo mikononi wa wanyonge wengi ambao kama wakiwa makini basi mabadiliko yanawezekana.

Hapa tunachosema ni kuwa, ni kweli kabisa kuwa katiba ya jamuhuri ipo kimya kuhusu elimu ya juu lakini katiba huandikwa na watu na ni wakati huu umma wote uamue kutaka kuandikwa kwa katiba na ili nchi na yote yaliyomo yawe kwa ajili ya wote na si wachache wanaodhani umma huu ni wa wapumbavu


YANA MWISHO...