Friday, June 23, 2006

GHANA KATUKOMBOA WAAFRIKA

Wakati mwanablogu mkongwe Ndesanjo Macha wa jikomboe.com analalamika kuwa afika si kitu yaani ni sifuri kwa kila kitu anachokitazama yeye na hasa akatilia maanani eti aibu inayozikuta timu zetu ambazo baadhi zimetolewa katika raundi za makundi

Jana Ghana wamemdhihirishia kuwa afica ndiko mpira unachezwa kwani black star waliwachabanga vijana wa Joji Kichaka kwa mabao mawili kwa moja huku ushujaa ukionekana karibu katika kila sekta ya timu ya Ghana hongera kwa wote na hasa kwa mashabiki tuliojitokeza kwa wingi kuwapa shavu vijana wa Africa.

Tunakutana na Brazil! Tutawashinda na ni bora nikasema kama kiungo mahiri wa Ghana Michel Essien alivyosema "tumecheza nao katika under 17 na 21, tunawajua kwani tuliwafunga bila kusubiri uda wa nyongeza" hakika brazil atapigwa bao 3-1 huku Appiah, na Essien wakifunga na Gyan bao kali la kichwa

SHANGILIA GHANA MABINGWA WAPYA WA KLD

Kwa ushindi huu Afrika imepata nafasi moja ya kuwa na timu ya 6 hapo 2010

3 comments:

Anonymous said...

Wameonyesha kile ambacho kila mwafrica alikuwa anakitarajia, safari ni ndefu lakini tutafika. Pengo la Essien lilionekana

Anonymous said...

Africa mpira twuweza sema kuna kitu kutojiamini na tunakosa mbinu bora za ufungaji cheki timu kama Ghana na Angola hawa walikuwa na uwezo wa kucheza nusu fainali

Anonymous said...

Huyo ndesanjo anachanganya mambo haoni marefa wanavyotubania, hawa ni wazungu anaokaa nao huko