UMEYAONA MABANGO WALIYOBEBA WASOMI WA UDSM WALIOSIMAMISHWA!!!!
Nimeingia katika blog ya Michuzi na kujionea mabango ambayo wanafunzi wa mwaka wa kwanza udsm waliandika wakishinikiza mkopo uwe 100%. Tazama hapa pembeni kushoto na bonyeza Michuzi, utajionea picha mbalimbali zilizopigwa kwa uzuri kabisa na gwiji la blog za picha nchini. Baadhi ya mabango hayo yanasema:-
SERIKALI PUNGUZENI SIASA KATIKA MASUALA YA MSINGI MNAUA ELIMU
KIKWETE UMESOMA BURE LEO UNATUDAI40%
KIKWETE BAADA YA WAKULIMA KUKUCHAGUA NDIVYO UNAVYOWALIPA
NASI TUUNDIWE KAMATI KAMA YA MALIMA NA MENGI halafu tupewe Milioni 100
Yapo mengi lakini haya ndo yamenivutia
2 comments:
Ebwana hawa jamaa wa serikali wanajifanya wababe sasa ngoja vijana tuwaonyeshe kazi.Ni hivi majuzi raisi wa south africa hon thabo mbeki alihutubia wanafunzi na kudai kwamba "in any country radical movement for development zinaanzia vyuo vikuu" sasa let us show them fedha zipo na vijana tunaweza tukasoma,tatizo serikali yetu imekuwa ya kujuana sana na kiushikaji tutafika kweli!ndiyo maana kunaufujaji mkubwa wa mabilioni ya shilingi serikalini ambayo ama kwa hakika isingekuwa ushkaji na kujuana yanatosha kabisa wanafunzi wote kusoma! ama kwa hakika mgomo huu ni wa haki na ni lazima matatizo haya yatatuliwe!
Unachosema Stive ni cha kweli kabisa kwani siku zote watu wanaojitambua ndio wa kwanza kuleta na kushawishi mabadiliko. Pesa zipo tena nyingi( si unakumbuka pesa za HIPC!)Lakini serikali hii inafanya kazi yake ikiwa hewani, kila siku safari ambazo hata manufaa hakuna. Elimu ya chuo kikuu sio lazima lakini wanaobahatika kuipata basi wasomeshwe kwani wengi huja kuitumikia jamii inayotozwa kodi
Post a Comment