Monday, December 18, 2006


CHUO KIKUU BILA MAKTABA!
Huu ni ukweli! Unashangaa chuo kimoja hapa mjini tena cha serikali kinatoa elimu ya juu bila kuwa na maktaba ambayo jengo lipo ila linakarabatiwa. Tunaunda wasomi wa vitini na madesa. Hii ndo bongo kila kitu usanii, fikiria mkandarasi wa kujenga jengo la wizara ya maendeleo ya jamii amemaliza jengo la ghorofa saba na kumshinda mkandarasi wa hapa chuoni ambaye alikuwa na kazi ya kukarabati milango na kupaka rangi, hii tenda ina walakini kwani wanaoumia ni wanaolipia huduma hii ya elimu na wanaofaidika na ukosefu wa maktaba ni wale waliosaini mkataba wa kuruhusu ukarabati.

Ukarabati umechukua miezi minne na sehemu na mpaka sasa hakuna kilichokabidhiwa kwa chuo ila jengo linang'aa kwa rangi nyeupe

2 comments:

Egidio Ndabagoye said...

Mashauri,

Kumbe upo siku nyingi sana.leo ndio nimekuona.Ungejisajili kule kwenye ukurasa wa wiki.

Nakukaribisha leo.Karibu sana utupe mambo ya hapo Kivukoni ya Zamani.

Anonymous said...

Siamini kabisa. Mwaka 2006, tunakaribia 2007, tuna chuo kisicho na maktaba? Usanii. Usanii. Usanii.