KUPANDA KWA ADA MNMA KUNAENDANA NA BAJETI YA KIKWETE?
Linaweza kuwa kama swali la mtu aliyechoka kufikiri. Nimewahi kukuandikia kuhusu kupanda kwa ada hapa chuoni kulikotangazwa na kaimu mkuu wa chuo kama ilivyoamliwa na kikao cha bodi ya chuo hiki chenye jina la muasisi wa taifa hili na aliyekuwa anataka kila mwanachi asome maana yake ni kuwa ada ya masomo iendane na uwezo halisi wa mtanzania wa kawaida.
Sio vibaya kujifikiria kitu ambacho wenzako wanaweza kukufikiria vinginevyo lakini kwa suala la ada kupanda hapa chuoni linamgusa kila mtu anayetoa pesa ili kupata elimu. Inawezekana kabisa waliopandisha ada (bodi) walikuwa na sababu kubwa na za msingi huku wakisaidiwa na utafiti walioufanya kana kwamba kutoza ada kubwa ndo kuonekana chuo bora
Lakini inawezekana kuwa wao kama wao na mishahara yao hawaoni tatizo na ada hii mpya kwani kama watu wanakaa kikao kwa siku na kulipana posho sawa na mshahara na marupurupu ya mwezi ya askari ada hii kwao ni ndogo na ni aibu kuilipa kana kwamba mwalimu alikuwa anafanya biashara ya elimu.
Pia labda bodi ilijua kwamba rais ataongeza mishahara na ndiyo maana ikaamua kuongeza ada ili kutorahisisha maisha kwa namna yoyote na hasa ukizingatia kuwa chuo hiki kipo katika ilani ya ccm katika mkakati wake kukiwezesha na kukikarabati!
Nakaribisha maoni kuhusu suala la kupanda kwa ada. Nenda sehemu iliyoandikwa comment bonyza na andika maoni yako na uyatume. Karibu
2 comments:
Kwa sasa kila kitu kinashangaza unachosema ni kweli kwani sioni haja ya kupandisha ada kwa nchi ambayo bado inahitaji wasomi wa kuweza kuingia katika dunia ya utandawazi
Ada! Hao wanaokaa kwenye bodi watoto wao wanasoma Ulaya na marikani sasa kapuku wewe kusoma ni kuwaletea fujo watoto wao watakapokuja nao kuchukua nafasi za baba zao. kazi nzuri endelea na tutapigana mpaka wajue nasi tunasehemu ya kutoa dukuduku letu
Post a Comment