Wednesday, July 12, 2006

BAHATI NASIBU YA MWALIMU NYERERE!!!

Nadhani sasa kila kitu kinafanywa ize isivyo kawaida, umeisikia hii bahati nasibu ya mwalimu!

Inawezekana jina la mwalimu sasa likawa ni ulaji, kama na wewe unachochote unachotaka faida basi andika mswada na tumia jina la mwalimu utapata pesa ule na unywe

3 comments:

Anonymous said...

Kumbe na wewe umeliona hilo!Jina la mwl sasa ni deal kubwa we si unaona wanavyozichanga kwa kisingizio cha kuondoa umaskini! Umaskini gani wa kuondolewa na bahati nasibu! Huu ni ukichaa unaoshabikiwa na majuha

Anonymous said...

Bahati nasibu si mbaya lakini wangetafuta njia nyingine ya kuuingizia pesa mfuko wa mwalimu na si kwa kuwaibia wanyonge. Mwalimu ana machapisho mengi tu tena ya maana hayo yangetayarishwa na tukauziwa

Anonymous said...

Deal hilo mwanangu wewe tu umelala. Changamka hata blog yako unaweza kuita Nyerere na ukatutaka wasomaji tulipie. Mjini hapa