Monday, August 07, 2006

KIKWETE KAPOTOSHWA KUHUSU 'MAPANKI'

Watu wanayala sana na hao sato anaowasema wanaliwa na watu wenye uwezo kama wale waliompotosha kwa kusema kuwa wakazi wa mwanza hawali mapanki, wasaidizi wake wamemwingiza mkenge kwa nia tu ya kulinda vibarua vyao.

Mapanki ndo kitoweo cha wengi hasa waliovijijini.

Hii ndo hulka ya viongozi wengi, wanafikiri wao wanapokula vizuri na kusaza nasi twala na kutabasamu.

Sauper hajakosea hata kidogo kila alichokionyesha ni sahihi kwa sisi tunaoijua mwanza na vijiji vyake

1 comment:

Rama Msangi said...

jambo pekee ninalolisubiri ni kuona namna Kikwete atawashughulikia waliomdanganya, kwasababu kudanganya kwa mujibu wa sheria ni kosa la jinai.

japo nina wasiwasi pia kuwa huenda ushabiki na unafiki wa wanasiasa wetu na hususan wabunge huenda ukazidi kumpotosha maana anawasikiliza zaidi na sio kujaribu kuchimba mwenyewe kuuona ukweli, ndio maana kule kwangu nimemshauri atembelee Kanyama aione