DALADALA NA WANAFUNZI!!!!Kama kuna mji ambao wanafunzi wanakuwa na wakati mgumu wa kwenda na kutoka shuleni ni Dar. Hii ni kwa sababu namba kubwa ya wanafunzi hawa wanasoma shule za kutwa zilizo mbali hivyo kuwafanya wategemee usafiri wa daladala kwani serikali ya Dar haitoi maelezo ya kutosha kuhusu mradi wa magari ya wanafunzi.
Juzi nimepanda daladala na nikashuhudia sheshe zito kati ya kondakta na 'dent' Hakuna aliyetaka kushindwa kila mmoja alikuwa ni mbabe kwa mwenzake konda anataka nauli ya mtu mzima na denti anatoa 50/=na kitambulisho cha shule anayosoma. Tafrani inaishia kwa abiria kuwa upande wa dent na kila kitu kikawa kama kawaida.
Inanikumbusha wakati ninasoma sekondari na siku moja nikampa konda50/= na kitambulisho cha shule niliyosoma Ndanda (Naleo Pasona en grata, Mwaimu, Limbu, na wengi najua mnaikumbuka shule hii) kumpa kitambulisho akashangaa na kuniuliza kama Ndanda Kosovo ( mwanamuziki wa wajelajela) kama ana shule. Sikutaka kumjibu kwani ni mazoea kwa konda na denti kila mtu kumtegea mwenzake nani aanze kutoa kashfa inayofuatiwa na vita kali ya maneno baini ya wawili.
Bahati nzuri mzee mmoja wa makamo akamshangaa konda kwa kutofahamu hata shule ambayo rais mstaafu Ben Mkapa aka Mr Clean alisoma, konda ulimi ukakatwa nami nikatulia kwa kujiamiani kituo kilichofuata nikashuka.
Nadhani ni wakati muafaka kwa wanadar kujadili ni kwa vipi tatizo la usafiri wa wanafunzi linaweza kutatuliwa pia na mikoa mingine, kila mmoja ashiriki bila kujali ni nani na ana nini!
Jumatatu njema ya pasaka