Asubuhi inapoanza na jua tamu kuchomoza basi pana shaka mchana wa jua unakaribia ukiita jioni kwa sauti kavu kama mtu asiyekunywa maji, na haya ndiyo Machweo yenyewe ambayo mtu hukaa na wenzake kutafakari nini amefanya kwa mchana na apange nini kwa kesho inayosadifiwa na nyota zinazoonekana kwa wingi
Friday, August 27, 2010
MAMISS WA SIKU HIZI KWA MIWANI..!!
Baadhi ya washiriki wa Vodacom Miss Tanzania wakiwa na miwani kitu ambacho kimekua kivutio kikubwa kwa mamiss,kiukweli zinawapendeza na kuwaongezea nakshi mida frlani hivi....
BINGWA WA MCHEZO WA GOLF DUNIANI TIGER WOODS AMETALIKIANA NA MKEWE ELIN NORDEGREN. HIZI NI HABARI KUTOKA MTANDAO WA MCHEZAJI GOLF NAMBA MOJA DUNIANI.
KWA PAMOJA WALISEMA "Tunasikitika kuwa ndoa yetu imefikia tamati na tunatakiana kila la heri katika mustakabala wetu," WAWILI HAO WALISEMA.
HATA HIVYO WAWILI HAO WAMESEMA WATASAIDIANA MAJUKUMU YA KULEA WATOTO WAO WAWILI. SUALA LA KUGAWANA PESA HALIJAWEKWA WAZI LAKINI TAARIFA KATIKA VYOMBO VYA HABARI VYA MAREKANI ZINASEMA KUWA BI.NORDEGREN HUENDA AKAONDOKA NA KITITA CHA DOLA MILIONI 100.
No comments:
Post a Comment