Wednesday, September 01, 2010


TENDWA KUTOA MAAMUZI PINGAMIZI LA CHADEMA BAADA YA SIKU TANO!

 
 
Na Mary Kweka –Maelezo
Msajili wa Vyama Vya Siasa Nchini John Tendwa amesema atatoa uamuzi wake dhidi ya malalamiko yaliyowasilishwa ofisini kwake jana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA)kuhusu mgombea wa urais kupitia chama cha mapinduzi(CCM) baada ya siku tano.
Bwana Tendwa ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari hayo ofisini kwake jijini Dar es salaam baada ya kupokea malalamiko hayo rasmi leo.
‘’Nitatoa maamuzi hayo baada ya kupokea maelezo kutoka kwa mlalamikiwa dhidi ya malalamikaji yaliyowasilishwa,na nitatoa nakala ya maamuzi kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi,Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi na Katibu Mkuu wa chama cha CHADEMA’’,Alisema Tendwa.
Akifafanua suala hilo Tendwa amesema baada ya maamuzi yake mlalamikaji na mlalamikiwa kama hawataridhika na uamuzi wake wanayo haki ya kwenda kutafuta haki yao kwenye vyombo vya sheria.
Aidha Msajili huyo Vyama ameongeza kuwa amepokea malalamiko hayo kwa mujibu wa sheria ya gharama za uchaguzi inachomkataza mgombea yeyote ambaye yeye mwenyewe, wakala wake au Chama chake kitafanya kitendo ambacho kimekatazwa kama ilivyoelekezwa kwenye sheria hiyo atakuwa au kitakuwa kimepoteza sifa za kushiriki mchakato wa uteuzi au uchaguzi.
Pingamizi hilo liliwasilishwa jana ofisi ya masajili huyo na Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika wakimlalamikia Mgombea urais wa chama cha mapinduzi Jakaya Mrisho Kikwete kutumia madaraka yake kutoa ahadi kwenye kampeni na kutangaza nyongeza ya mshahara kwa wafanyakazi wakati wa kampeni.

No comments: