Monday, June 23, 2008

USISEME UNA MATATIZO

Wadau hii nimeitoa kwa Mzee wa Sumo.

Mzee Kidevu kanitumia hii!Jamaa wawili walikutana kwenye kituo cha basi wakafanya mazungumzo.

Mmoja aling'ang'nia kuzungumzia kero za familia yake hatimaye mwenzake akasema " Unadhani familia yako ina matatizo?"Basi sikiliza kisa hiki.

"Miaka michache iliyopita nilikutana na mwanamke mjane aliyekua na binti mkubwa tu na tukaamua kuoana. Baadaye baba yangu akamuoa binti yangu wa kambo hivyo huyo binti yangu wa kambo akawa mama yangu wa kambo na Baba yangu akawa mtoto wangu wa kambo wa kiume ambapo mke wangu akawa mama mkwe wa mkwe wake.Baadaye binti yamke wangu yaani binti yangu wa kambo alipata mtoto wa kiume. mtoto huyo wa kiume alikua ndugu yangu kwa sababu tulichangia baba mmoja. lakini kwa vile alikua ni mtoto wabinti wa mke wangu papo hapo akawa mjukuu wa mke wangu na mimi nikawa babu yake ndogo wangu.

Lakini hayo yote yalikua si kitu mpaka mimi na mke wangu tulipopata mtoto wa kiume. Sasa msichana ambaye ni ndugu wa mtoto wangu huyo wa kiume kwa kuchangia mama yao mmoja, akawa pia bibi yake. Hali hiyo ilimfanya pia baba yangu kua shemeji wa mtoto wangu ambaye ndugu yake wa kike kwa upande wa mama yao ndie mke wake baba yangu. Kwa hiyo mimi ni shemeji yake mama yangu wa kambo ambapo mke wangu ni mama mdogo (anti) wabinti yake mwenyewe . Mtoto wangu wa kiume ni mpwa wa baba yangu ambapo mimi nikawa babu yangu mwenyewe.

SWALI.Je, unadhani mpaka hapo wewe una matatizo ya kifamilia? Acha kulalamika

No comments: