Monday, June 23, 2008

MAXIMO ANA MCHANGO MDOGO SANA KATIKA SOKA LA TANZANIA

Najua wapo wanaoamini kuwa ufanisi wa Taifa Starz umechangiwa na kocha wa kibrazil aliyeletwa na JK. Kwangu mimi hali ni tofauti na wote wanaotangaza kuwa Tanzania imetangazwa na Maximo.

Kuna vitu kama viwili ambavyo ndivyo vimeifanya Taifa stars ifikie kiwango hiki ambacho hata hivyo hakijafikia kiwango kilichooneshwa na timu yetu ya taifa kwenye miaka ya 80. Vitu hivi ni kama vifuatavyo:-

Sapoti kubwa ya serikali kwa timu: Hii ndiyo chachu kubwa sana ya timu yetu kufanya vizuri. Wakati mbrazil anakuja si kweli kuwa timu yetu ilikuwa mbovu kiasi cha kusema kwamba alitukuta tuko wodi ya wagonjwa mahututi. serikali miaka ile baada 80 haikuonesha kipaumbele katika kusaidia timu ya taifa. Rais JK alipoingia madarakani kuliendana na mabadiliko makubwa katika utendaji wa TFF (zamani FAT) na hivyo alitambua kiu wa watanzania kuwa ni maendeleo ya soka na hapo ndipo alipoanza kuisadia timu kwa kuipatia kocha na misaada mingine.

Mfumo wa soka letu ulitengemaa na shurani kubwa ziende kwa shule mbalimbali nchini ambazo zilikuwa stari wa mbele kuwapa nafasi vijana wenye vipaji vya soka kujiunga na shule hizo na kuendeleza vipaji vyao, mfano wa shule hizo ni Makongo na Jitegemee kwa DSM. Mikoani napo vijana wenye vipaji walikuwa wanaangaliwa kwa ukaribu zaidi.

Kutokana na muundo mzima wa uongozi wa chama cha soka Tz wadau mbalimbali walijitokeza kuisadia timu ya taifa kwa hali na mali kama tunavyoshuhudia wafadhili mbalimbali ambao wamekuwa wakitoa pesa zao na kudhamini timu ya taifa. Kwa kuwataja kwa uchache hawa ni TBL, Serengeti, NMB na NBC pamoja na makampuni na watu binafsi.

Ukiangalia sababu hizi utagundua kabisa hata walimu wetu wa bongo wangekuwa wakipewa sapoti kama hii wasingeshindwa kuifikisha timu hii hapa ilipo.

Unaweza kufikiria hili na kutoa maoni yako

No comments: