Thursday, April 17, 2008

UNAFIKI WA VIONGOZI WA DINI

Siongelei dhehebu moja ama mawili, naongelea viongozi wa dini zote za kigeni( ambazo hazina asili yake Afrika).

Makanisa yetu na misikiti yetu imekuwa ikipokea misaada mbalimbali toka kwa wafadhili wa ndani na nje. Misaada hii imekuwa ni kwa ajili ya maendeleo ya waumini wote.

Cha ajabu sasa ambacho msomaji unaweza kukubaliana nami ni kuwa, misaada hii imekuwa ikiishia matumboni mwa viongozi hawa ambao unapokutana nao njiani na maneno yao huku wakiosha mikono kila wanapoongea ni tofauti kabisa na matendo yao ya KIFISADI.

Tunapoongelea kuhusu ufisadi kwa viongozi wa serikali basi tusisahau kile kinachofanywa na viongozi wetu wanaovaa majoho na kanzu nzuri

2 comments:

Anonymous said...

Hakika viongozi wa dini ni wanafiki kwa kwenda mbele.Mdau UK

Anonymous said...

wengine Allah hatotuhukumu na moto, tutachwapa viboko 60 na kuongezewa 15 na kuambiwa nendeni mkale pepo.

Murokozi