Thursday, April 17, 2008

UNAFIKI WA VIONGOZI WA DINI

Siongelei dhehebu moja ama mawili, naongelea viongozi wa dini zote za kigeni( ambazo hazina asili yake Afrika).

Makanisa yetu na misikiti yetu imekuwa ikipokea misaada mbalimbali toka kwa wafadhili wa ndani na nje. Misaada hii imekuwa ni kwa ajili ya maendeleo ya waumini wote.

Cha ajabu sasa ambacho msomaji unaweza kukubaliana nami ni kuwa, misaada hii imekuwa ikiishia matumboni mwa viongozi hawa ambao unapokutana nao njiani na maneno yao huku wakiosha mikono kila wanapoongea ni tofauti kabisa na matendo yao ya KIFISADI.

Tunapoongelea kuhusu ufisadi kwa viongozi wa serikali basi tusisahau kile kinachofanywa na viongozi wetu wanaovaa majoho na kanzu nzuri
UTAJIRI WA CHENGE

Kama kuna jambo ambalo linaongelewa sana kwa sasa hapa kwetu Tanzania ni suala zima la utajiri wa Chenge ambaye aliwahi kuwa mwanasheria mkuu wa serikali kwa kipindi cha miaka 10 katika zama za Mkapa.

Ni katika kipindi hiki ndipo taifa lilishuhudia uingiwaji mkubwa wa mikataba ambayo leo ndio inawasumbua watanzania.

Mikataba hii haikufungwa na kina chifu Mangungo bali ilifungwa na wasomi mahiri kabisa na wengine waliosoma vizuri katika vyuo vikubwa kabisa duniani na tena wakilipiwa na wanachi masikini kwa lengo moja tu kubwa, kuwatetea wananchi katika mambo mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.

Lakini sasa tunachoshuhudia ni kinyume cha yale tuliyoamini, wale tuliowasomesha wamekuwa ni vinara wakubwa wa ufisadi na wamejaa viburi kiasi kwamba mtu anasema hawezi kuachia ngazi/madaraka kwa kelele za wananchi, swali langu hapa ni hili,

Hivi Mtanzania ni nani katika Tanzania!