Tuesday, January 27, 2009

HIVI MWISHO WA MZAZI MASKINI WA TZ NI NINI!!


Kichwa hapo juu kisikustue na kukutisha, umaskini ninaoungelea hapa sio ule unaojua wewe wa kukosa kula, malazi, hapa naongelea kuhusu uwezo wa umma kufanya maamuzi yao yanaowahusu.

Umma ni tofauti sana na wapiga kura, hawa wapo kwa ajili ya kutunisha matumbo yao. Umma ni zaidi ya watu kwani unahusisha mazingira yao na si kukumbukana kwa baada ya miaka mitano.

Fikiria sakata la vyuo vikuu linaloendelea hivi sasa huku asilimia kubwa ya wanafunzi (wengi wao ni watoto wa wakulima vijijini) ikiwa imekosa udahiliwa mpya uliokuja kama wokovu kwa watoto wa matajiri.

Nadhani ni wakati wa umma kuamka na kutambua kuwa amani bila haki ni kama mawingu bila mvua na siku zote haki hutafutwa. Mustakabali wa Tanzania upo mikononi wa wanyonge wengi ambao kama wakiwa makini basi mabadiliko yanawezekana.

Hapa tunachosema ni kuwa, ni kweli kabisa kuwa katiba ya jamuhuri ipo kimya kuhusu elimu ya juu lakini katiba huandikwa na watu na ni wakati huu umma wote uamue kutaka kuandikwa kwa katiba na ili nchi na yote yaliyomo yawe kwa ajili ya wote na si wachache wanaodhani umma huu ni wa wapumbavu


YANA MWISHO...