Asubuhi inapoanza na jua tamu kuchomoza basi pana shaka mchana wa jua unakaribia ukiita jioni kwa sauti kavu kama mtu asiyekunywa maji, na haya ndiyo Machweo yenyewe ambayo mtu hukaa na wenzake kutafakari nini amefanya kwa mchana na apange nini kwa kesho inayosadifiwa na nyota zinazoonekana kwa wingi
Wednesday, December 30, 2009
SAFU ZA MILIMA YA KITONGA: UZOEFU NA PICHA
Kwa muda wa kama wiki mbili nilikuwa mkoani Iringa kwa ajili ya kushiriki katika michezo inayohusisha taasisi za elimu ya juu na vyuo nchini.
Nilishiriki katika mchezo wa mpira wa wavu, nitajaribu kupandisha picha za michezo hiyo lakini pia nitaweka picha za safu za milima ya Kitonga

Wednesday, June 17, 2009
JENGO HILI NDIMO TUNATEGEMEA WABUNGE WATUWAKILISHE KIKAMILIFUBAJETI YA 2009/10
Wakati serikali na Kikwete wakijisifu kwa kuweka kipaumbele katika kilimo, ukweli ni kwamba hakuna jipya linalofanywa na seriakli katika kuhakikisha kuwa kilimo kinakuwa cha kwanza, ni kutumia maneno mazuri kama mawingu makubwa yasiyoleta mvua, huwezi kusema KILIMO KWANZA ilhali umetenga asilimia 6.9 kwa ajili ya kilimo huku AU ikisisitiza angalau kilimo kitengewe asilimia kuanzia 10
Thursday, June 04, 2009
Saturday, May 23, 2009
Monday, May 11, 2009
Kwa mujibu wa TFF, shirikisho la soka nchini lilimwomba Maximo atafute makocha, na hawa ndo aliowaleta. Swali hivi maximo ni kocha ama wakala wa kutafuta makochaMAXIMO HATUFAI
Wengi unapomwongelea huyu jamaa husingizia kuwa watz wanamwonea wivu, sio kweli maximo hafai kuwa kocha wa timu ya taifa ya Tanzania. Najua msomaji unaweza kutoa mengi, hapa ni changamoto tu na ni wakati wako wewe kuchangia
Tuesday, January 27, 2009
HIVI MWISHO WA MZAZI MASKINI WA TZ NI NINI!!
Kichwa hapo juu kisikustue na kukutisha, umaskini ninaoungelea hapa sio ule unaojua wewe wa kukosa kula, malazi, hapa naongelea kuhusu uwezo wa umma kufanya maamuzi yao yanaowahusu.
Umma ni tofauti sana na wapiga kura, hawa wapo kwa ajili ya kutunisha matumbo yao. Umma ni zaidi ya watu kwani unahusisha mazingira yao na si kukumbukana kwa baada ya miaka mitano.
Fikiria sakata la vyuo vikuu linaloendelea hivi sasa huku asilimia kubwa ya wanafunzi (wengi wao ni watoto wa wakulima vijijini) ikiwa imekosa udahiliwa mpya uliokuja kama wokovu kwa watoto wa matajiri.
Nadhani ni wakati wa umma kuamka na kutambua kuwa amani bila haki ni kama mawingu bila mvua na siku zote haki hutafutwa. Mustakabali wa Tanzania upo mikononi wa wanyonge wengi ambao kama wakiwa makini basi mabadiliko yanawezekana.
Hapa tunachosema ni kuwa, ni kweli kabisa kuwa katiba ya jamuhuri ipo kimya kuhusu elimu ya juu lakini katiba huandikwa na watu na ni wakati huu umma wote uamue kutaka kuandikwa kwa katiba na ili nchi na yote yaliyomo yawe kwa ajili ya wote na si wachache wanaodhani umma huu ni wa wapumbavu
YANA MWISHO...

Saturday, December 27, 2008
Thursday, October 09, 2008
USISHANGAE! HATA HILI LINAWEZA KUWA KWELI
Nimeipata toka kwa mdau mmoja na nimeona na wewe nikufahamishe.
Familia moja ilishangazwa pale walipopokea jeneza la marehemu mama yao aliyefariki nchini Marekani. Lilitumwa na mmoja ya watoto wake wa kike. Mwili ndani ya jeneza ulikuwa umesongwa sana ndani ya jeneza kiasi kwamba uso wa marehemu ulikuwa umegusa kioo cha jeneza! Walipofungua jeneza, walikuta barua juu ya merehemu, iliyosomeka namna hii: 'Wapendwa ndugu zangu, nimeutuma mwili wa mama yetu kwa ajili ya mazishi, kwani imekuwa siku zote hamu yake kubwa kuzikwa nyumbani Ileje, katika nyumba ya ukoo. Samahani sikuweza kuja na mwili kwani nimenyimwa likizo kwani kuna upungufu wa wafanyakazi hapa kazini mwezi huu. Ndani ya jeneza, chini ya mwili wa mama, kuna makopo 12 ya samaki wa makopo, paketi 10 za supu ya Royco na chupa 8 za jam ya maembe.Mgawane hivi kwa jinsi mtakavyoamua nyinyi. Katika miguu ya mama kuna pea moja ya viatu vya Reebok namba 9 kwa ajili ya mtoto mkubwa wa Mwakajinga. Pia, kuna pea mbili za viatu kwa ajili ya watoto wa Mwakipesile na Ipiana , natumaini nitakuwa sijakosea namba za miguu. Nimemvalisha pia mama American T-shirts 6, kubwa kabisa ni kwa ajili ya Mwakibibi, na zinazobaki ni za watoto wake. Hizo jeans mpya 2 ambazo mama amezivaa ni za wavulana Mwakatumbula na Mwakitobe. Hiyo Swiss watch mkono wake wa kushoto ni zawadi ya Rhoida kwa ajili ya sikukuu yake ya kutimiza miaka 21. Anti Queen, hizo heleni, mkufu na pete ambazo mama amevaa ni zako. Hizo soksi 6 ambazo mama amevaa wagaiwe wajomba. Tafadhali mgawane kama nilivyosema na kama kuna kitu kingine mnahitaji, basi mnieleze kwani hali ya baba nayo siku hizi si nzuri sana .Dada yenu mpenzi, Mama Mpoki

Monday, June 23, 2008
MAXIMO ANA MCHANGO MDOGO SANA KATIKA SOKA LA TANZANIA
Najua wapo wanaoamini kuwa ufanisi wa Taifa Starz umechangiwa na kocha wa kibrazil aliyeletwa na JK. Kwangu mimi hali ni tofauti na wote wanaotangaza kuwa Tanzania imetangazwa na Maximo.
Kuna vitu kama viwili ambavyo ndivyo vimeifanya Taifa stars ifikie kiwango hiki ambacho hata hivyo hakijafikia kiwango kilichooneshwa na timu yetu ya taifa kwenye miaka ya 80. Vitu hivi ni kama vifuatavyo:-
Sapoti kubwa ya serikali kwa timu: Hii ndiyo chachu kubwa sana ya timu yetu kufanya vizuri. Wakati mbrazil anakuja si kweli kuwa timu yetu ilikuwa mbovu kiasi cha kusema kwamba alitukuta tuko wodi ya wagonjwa mahututi. serikali miaka ile baada 80 haikuonesha kipaumbele katika kusaidia timu ya taifa. Rais JK alipoingia madarakani kuliendana na mabadiliko makubwa katika utendaji wa TFF (zamani FAT) na hivyo alitambua kiu wa watanzania kuwa ni maendeleo ya soka na hapo ndipo alipoanza kuisadia timu kwa kuipatia kocha na misaada mingine.
Mfumo wa soka letu ulitengemaa na shurani kubwa ziende kwa shule mbalimbali nchini ambazo zilikuwa stari wa mbele kuwapa nafasi vijana wenye vipaji vya soka kujiunga na shule hizo na kuendeleza vipaji vyao, mfano wa shule hizo ni Makongo na Jitegemee kwa DSM. Mikoani napo vijana wenye vipaji walikuwa wanaangaliwa kwa ukaribu zaidi.
Kutokana na muundo mzima wa uongozi wa chama cha soka Tz wadau mbalimbali walijitokeza kuisadia timu ya taifa kwa hali na mali kama tunavyoshuhudia wafadhili mbalimbali ambao wamekuwa wakitoa pesa zao na kudhamini timu ya taifa. Kwa kuwataja kwa uchache hawa ni TBL, Serengeti, NMB na NBC pamoja na makampuni na watu binafsi.
Ukiangalia sababu hizi utagundua kabisa hata walimu wetu wa bongo wangekuwa wakipewa sapoti kama hii wasingeshindwa kuifikisha timu hii hapa ilipo.
Unaweza kufikiria hili na kutoa maoni yako

USISEME UNA MATATIZO
Wadau hii nimeitoa kwa Mzee wa Sumo.
Mzee Kidevu kanitumia hii!Jamaa wawili walikutana kwenye kituo cha basi wakafanya mazungumzo.
Mmoja aling'ang'nia kuzungumzia kero za familia yake hatimaye mwenzake akasema " Unadhani familia yako ina matatizo?"Basi sikiliza kisa hiki.
"Miaka michache iliyopita nilikutana na mwanamke mjane aliyekua na binti mkubwa tu na tukaamua kuoana. Baadaye baba yangu akamuoa binti yangu wa kambo hivyo huyo binti yangu wa kambo akawa mama yangu wa kambo na Baba yangu akawa mtoto wangu wa kambo wa kiume ambapo mke wangu akawa mama mkwe wa mkwe wake.Baadaye binti yamke wangu yaani binti yangu wa kambo alipata mtoto wa kiume. mtoto huyo wa kiume alikua ndugu yangu kwa sababu tulichangia baba mmoja. lakini kwa vile alikua ni mtoto wabinti wa mke wangu papo hapo akawa mjukuu wa mke wangu na mimi nikawa babu yake ndogo wangu.
Lakini hayo yote yalikua si kitu mpaka mimi na mke wangu tulipopata mtoto wa kiume. Sasa msichana ambaye ni ndugu wa mtoto wangu huyo wa kiume kwa kuchangia mama yao mmoja, akawa pia bibi yake. Hali hiyo ilimfanya pia baba yangu kua shemeji wa mtoto wangu ambaye ndugu yake wa kike kwa upande wa mama yao ndie mke wake baba yangu. Kwa hiyo mimi ni shemeji yake mama yangu wa kambo ambapo mke wangu ni mama mdogo (anti) wabinti yake mwenyewe . Mtoto wangu wa kiume ni mpwa wa baba yangu ambapo mimi nikawa babu yangu mwenyewe.
SWALI.Je, unadhani mpaka hapo wewe una matatizo ya kifamilia? Acha kulalamika

HIVI IKIWA NDIVYO, ITAKUWAJE!!!
Hii nimeipata toka kwa rafiki yangu aliyeko Nairobi na ninapenda kuiweka hapa kama ilivyoletwa
Kuna mdau eti laleta hii, jamani kutania viongozi...
Nafurahi kuwajulisheni nyote kwamba kuna vyuo kumi vimefunguliwa maeneo mbalimbali nchini, vikitoa kozi mbalimbali na kubeba majina ya watu maarufu kama ifuatavyo:
* Benjamin Mkapa Institute of Political Entrepreneurship and Openness
* David Balali School of Central Banking and Foreign Debt Management
* Andrew Chenge College of Applied Contractual Law
* Ali Hassan Mwinyi University of Inflation Control
* Karamagi Institute of Mining Licensing and Administration of Mining Contracts
* Zakia Meghji college of Tourism and Protection of Public Funds and Natural Resources
* Ditopile Mzuzuri School of Conveyance and Welfare of Public Drivers
* Mwalimu Nyerere University College of Privatization
* Mkono Intitute of Legal Fraud Prevention
* Lowassa School of Prevention of Fake Companies
Mimi nimefurahishwa na utani huu, sijui wewe

Thursday, April 17, 2008
UNAFIKI WA VIONGOZI WA DINI
Siongelei dhehebu moja ama mawili, naongelea viongozi wa dini zote za kigeni( ambazo hazina asili yake Afrika).
Makanisa yetu na misikiti yetu imekuwa ikipokea misaada mbalimbali toka kwa wafadhili wa ndani na nje. Misaada hii imekuwa ni kwa ajili ya maendeleo ya waumini wote.
Cha ajabu sasa ambacho msomaji unaweza kukubaliana nami ni kuwa, misaada hii imekuwa ikiishia matumboni mwa viongozi hawa ambao unapokutana nao njiani na maneno yao huku wakiosha mikono kila wanapoongea ni tofauti kabisa na matendo yao ya KIFISADI.
Tunapoongelea kuhusu ufisadi kwa viongozi wa serikali basi tusisahau kile kinachofanywa na viongozi wetu wanaovaa majoho na kanzu nzuri

UTAJIRI WA CHENGE
Kama kuna jambo ambalo linaongelewa sana kwa sasa hapa kwetu Tanzania ni suala zima la utajiri wa Chenge ambaye aliwahi kuwa mwanasheria mkuu wa serikali kwa kipindi cha miaka 10 katika zama za Mkapa.
Ni katika kipindi hiki ndipo taifa lilishuhudia uingiwaji mkubwa wa mikataba ambayo leo ndio inawasumbua watanzania.
Mikataba hii haikufungwa na kina chifu Mangungo bali ilifungwa na wasomi mahiri kabisa na wengine waliosoma vizuri katika vyuo vikubwa kabisa duniani na tena wakilipiwa na wanachi masikini kwa lengo moja tu kubwa, kuwatetea wananchi katika mambo mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.
Lakini sasa tunachoshuhudia ni kinyume cha yale tuliyoamini, wale tuliowasomesha wamekuwa ni vinara wakubwa wa ufisadi na wamejaa viburi kiasi kwamba mtu anasema hawezi kuachia ngazi/madaraka kwa kelele za wananchi, swali langu hapa ni hili,
Hivi Mtanzania ni nani katika Tanzania!

Subscribe to:
Posts (Atom)